Vigezo na Masharti · Terms and Conditions
Ilisasishwa mwisho: 16 Septemba 2026 · English version below
Karibu kwenye tovuti ya Lilac Labs.
Kwa kuingia au kutumia tovuti yetu lilaclabs.shop na kununua bidhaa zetu, unakubali kufungwa na Vigezo na Masharti haya (“Masharti”). Ikiwa hukubaliani na sehemu yoyote ya Masharti haya, tafadhali usitumie tovuti au huduma zetu.
1. Taarifa za Biashara
Tovuti hii inaendeshwa na:
Jina la kampuni: Camp Lilac Mikumi Company Limited (chapa ya biashara: Lilac Labs)
Nchi ya uendeshaji: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Usajili: BRELA Na. 167521584 · TIN 167-521-584
Ofisi: Mbezi Beach, Dar es Salaam (Goba Road, karibu na Massana Hospital)
WhatsApp: +255 765 457 942
2. Sifa za Kutumia Tovuti
Kwa kutumia Tovuti hii, unathibitisha kwamba:
- Una umri wa angalau miaka 18, au
- Unatumia Tovuti chini ya usimamizi wa mzazi au mlezi halali.
3. Bidhaa na Taarifa
Tunafanya kila juhudi kuonyesha maelezo ya bidhaa, viambato, picha na bei kwa usahihi. Hata hivyo:
- Picha za bidhaa ni kwa ajili ya kuonyesha tu
- Rangi, vifungashio na muonekano vinaweza kutofautiana
- Tuna haki ya kubadilisha au kusitisha bidhaa wakati wowote bila taarifa
4. Tahadhari ya Afya na Virutubisho
Kwa bidhaa zetu zilizo virutubisho vya lishe au bidhaa za afya njema:
- Bidhaa zetu hazikusudiwi kutambua, kutibu, kuponya au kuzuia ugonjwa wowote
- Matokeo yanaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu
- Unapaswa kushauriana na mtaalamu wa afya aliyehitimu kabla ya kutumia kirutubisho chochote, hasa ikiwa wewe ni mjamzito, unanyonyesha, unatumia dawa au una tatizo la kiafya
- Tumia bidhaa kama ilivyoelekezwa kwenye lebo tu
5. Oda na Kukubaliwa kwa Oda
- Oda zote zinazowekwa kupitia Tovuti zinategemea kukubaliwa na upatikanaji wa bidhaa
- Tuna haki ya kukataa au kufuta oda yoyote kwa sababu yoyote, ikiwemo kuhisi udanganyifu, makosa ya bei au uhaba wa bidhaa
- Oda ikishawekwa, mratibu wetu wa delivery atakupigia simu (kutoka namba 0761 389 838 au 0654 226 299) au kukuandikia WhatsApp kuthibitisha oda yako. Oda inahesabika kuwa imekubaliwa baada ya uthibitisho huo
6. Bei na Malipo
- Bei zote zimeorodheshwa kwa Shilingi za Tanzania (TZS) isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo
- Bei zinaweza kubadilika wakati wowote bila taarifa ya awali
- Dar es Salaam, Arusha na Dodoma: unalipa dereva wakati wa kupokea mzigo (lipa ukipokea)
- Mikoa mingine: baada ya mzigo wako kupanda basi na kutumiwa picha ya risiti ya basi, unalipa kikamilifu kwa Lipa Namba 16429521 (LILAC LABS) kabla ya kuchukua mzigo ofisi ya basi
- Hatuwajibiki kwa ada za ziada zinazotozwa na benki yako au mtoa huduma wako wa malipo (kwa mfano ada za miamala ya simu)
7. Usafirishaji na Uwasilishaji
- Muda wa uwasilishaji ni makadirio tu na unaweza kubadilika kutokana na kuchelewa kwa usafirishaji, hali ya hewa au sababu nyingine zilizo nje ya uwezo wetu
- Hatuwajibiki kwa kuchelewa kunakosababishwa na taarifa zisizo sahihi za uwasilishaji zilizotolewa na mteja
- Hatari ya kupotea kwa mzigo huhamia kwa mteja pindi oda inapokabidhiwa kwa msafirishaji (dereva au kampuni ya basi)
8. Kurejesha Bidhaa na Kurejeshewa Pesa
Kurejesha bidhaa na kurejeshewa pesa kunaongozwa na Sera yetu ya Kurejeshewa Pesa, ambayo ni sehemu ya Masharti haya, ikiwemo dhamana ya kurejeshewa pesa ndani ya siku 30.
Tafadhali soma Sera ya Kurejeshewa Pesa kwa makini kabla ya kununua.
9. Haki Miliki
Maudhui yote kwenye Tovuti hii, yakiwemo lakini si tu:
- Nembo (logo)
- Majina ya chapa
- Maandishi
- Picha
- Michoro
- Miundo ya bidhaa
ni mali ya kiakili ya Camp Lilac Mikumi Company Limited (Lilac Labs) na hayaruhusiwi kunakiliwa, kuzalishwa upya, kusambazwa au kutumiwa bila ruhusa ya maandishi ya awali.
10. Ukomo wa Dhima
Kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria:
- Hatutawajibika kwa hasara yoyote isiyo ya moja kwa moja, ya bahati mbaya, maalum au inayotokana na matumizi yako ya Tovuti au bidhaa
- Dhima yetu yote haitazidi kiasi ulicholipa kwa bidhaa iliyosababisha dai husika
11. Mwenendo wa Mtumiaji
Unakubali kutofanya yafuatayo:
- Kutumia Tovuti kwa madhumuni yasiyo halali
- Kujaribu kupata ufikiaji usioruhusiwa wa Tovuti au mifumo yake
- Kutumia vibaya au kuingilia uendeshaji wa Tovuti
- Kutoa taarifa za uongo au za kupotosha
12. Faragha
Matumizi yako ya Tovuti pia yanaongozwa na Sera yetu ya Faragha, inayoeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako binafsi.
13. Mabadiliko ya Masharti Haya
Tuna haki ya kusasisha au kubadilisha Masharti haya wakati wowote.
Mabadiliko yatatumika mara moja yanapowekwa kwenye Tovuti. Kuendelea kutumia Tovuti kunamaanisha unakubali Masharti yaliyosasishwa.
14. Sheria Inayotumika
Masharti haya na mgogoro wowote unaotokana nayo yataongozwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
15. Mawasiliano
Ukiwa na swali lolote kuhusu Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi:
- 📱 WhatsApp: +255 765 457 942
- 🏢 Camp Lilac Mikumi Company Limited (Lilac Labs), Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania
English version
Last updated: 16 September 2026
Welcome to Lilac Labs website.
By accessing or using our website lilaclabs.shop and purchasing our products, you agree to be bound by these Terms and Conditions (“Terms”). If you do not agree with any part of these Terms, please do not use our website or services.
1. Business Information
This website is operated by:
Business Name: Camp Lilac Mikumi Company Limited
Country of Operation: United Republic of Tanzania
Registration: BRELA No. 167521584 · TIN 167-521-584
Office: Mbezi Beach, Dar es Salaam (Goba Road, near Massana Hospital)
WhatsApp: +255 765 457 942
2. Eligibility to Use the Website
By using this Site, you confirm that:
- You are at least 18 years old, or
- You are accessing the Site under the supervision of a parent or legal guardian.
3. Products and Information
We make every effort to display product descriptions, ingredients, images, and pricing accurately. However:
- Product images are for illustrative purposes only
- Colors, packaging, and appearance may vary
- We reserve the right to modify or discontinue products at any time without notice
4. Health & Supplement Disclaimer
If our products include dietary supplements or wellness products:
- Our products are not intended to diagnose, treat, cure, or prevent any disease
- Results may vary from person to person
- You should consult a qualified healthcare professional before using any supplement, especially if you are pregnant, nursing, taking medication, or have a medical condition
- Use products only as directed on the label
5. Orders and Acceptance
- All orders placed through the Site are subject to acceptance and availability
- We reserve the right to refuse or cancel any order for any reason, including suspected fraud, errors in pricing, or stock issues
- Once an order is placed, our delivery coordinator will call you (from 0761 389 838 or 0654 226 299) or message you on WhatsApp to confirm it. An order is deemed accepted once it has been confirmed this way
6. Pricing and Payment
- All prices are listed in TZS unless otherwise stated
- Prices may change at any time without prior notice
- Dar es Salaam, Arusha and Dodoma: you pay the driver when you receive your parcel (pay on delivery)
- Other regions: once your parcel has been placed on the bus and you have received the photo of the bus receipt, you pay in full to Lipa Namba 16429521 (LILAC LABS) before collecting the parcel at the bus office
- We are not responsible for additional fees charged by your bank, card issuer, or payment provider
7. Shipping and Delivery
- Delivery times are estimates only and may vary due to courier delays, customs, weather, or other factors beyond our control
- We are not responsible for delays caused by incorrect delivery information provided by the customer
- Risk of loss passes to the customer once the order is handed over to the courier
8. Returns and Refunds
- Returns and refunds are governed by our Refund & Return Policy, which forms part of these Terms.
- Please review the Refund & Return Policy carefully before making a purchase.
9. Intellectual Property
All content on this Site, including but not limited to:
- Logos
- Brand names
- Text
- Images
- Graphics
- Product designs
is the intellectual property of Camp Lilac Mikumi Company Limited (Lilac Labs) and may not be copied, reproduced, distributed, or used without prior written permission.
10. Limitation of Liability
To the fullest extent permitted by law:
- We shall not be liable for any indirect, incidental, special, or consequential damages arising from your use of the Site or products
- Our total liability shall not exceed the amount paid by you for the product giving rise to the claim
11. User Conduct
You agree not to:
- Use the Site for unlawful purposes
- Attempt to gain unauthorized access to the Site or systems
- Misuse or interfere with the Site’s operation
- Submit false or misleading information
12. Privacy
Your use of the Site is also governed by our Privacy Policy, which explains how we collect, use, and protect your personal information.
13. Changes to These Terms
We reserve the right to update or modify these Terms at any time.
Changes will be effective immediately upon posting on the Site. Your continued use of the Site constitutes acceptance of the updated Terms.
14. Governing Law
These Terms and any disputes arising from them shall be governed by and construed in accordance with the laws of the United Republic of Tanzania.
15. Contact Information
If you have any questions regarding these Terms, please contact us at:
- 📱 +255 765 457 942
- 📍 Camp Lilac Mikumi Company Limited (Lilac Labs), Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania